KATIBU MKUU WA CCM ATANGAZA KUMNG'OA MBUNGE WA CHADEMA WILFRED LWAKATARE

Katibu Mkuu wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Dkt. Bashiru Ally amewataka wanachama wa chama hicho kumuunga mkono Mbunge wa Bukoba Mjini (CHADEMA), Wilfred Lwakatare, ili aweze kumng'oa katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Akizungumza na baadhi ya wanachama na viongozi nje ya ofisi za CCM Mkoa wa Kagera, mjini Bukoba, jana Desemba 22, 2018 Dkt. Bashiru ametaja sababu za kumuunga mkono kuwa Wilfred Lwakatare ni Mbunge halali, muungwana na hapotoshi wananchi.

Hata hivyo, pamoja na sifa hizo alisema mbunge huyo ajiandae kung'oka mwaka 2020, huku akiagiza kabla ya kuondoka mkoani Kagera apatiwe maelezo ya sababu ya kufa kwa kilimo cha zao la chai alilodai lilikuwa mkombozi kwa wananchi ambao walifanikiwa kujiongezea kipato na kusomesha watoto.

Dkt. Bashiru amesisitiza kuwa Taifa lina uwezo wa kujitegemea huku akitaja baadhi ya changamoto zilizopo zikiwemo ukosefu wa ajira na kuagiza wakuu wa mikoa nchini kutatua kero za wananchi pamoja na kuondoa uonevu kwa wafanyabiashara wadogo.

Katibu mkuu huyo amesema amekwenda mkoani Kagera, ambako ni nyumbani kwake kwa ajili ya mapumziko ya mwishoni mwa mwaka yatakayokwenda sambamba na ziara hadi Januari 2, 2019 kwa kutembelea wilaya mbalimbali za mkoa huo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527