SERIKALI KUWASHUGHULIKIA WANAOTUMIA MAKANISA NA MISIKITI KUVURUGA AMANI


Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amesema Serikali haitawavumilia wanaotumia taasisi za dini ikiwamo misikiti na makanisa kuvuruga amani.

Alisema hayo juzi kwa niaba ya Rais John Magufuli wakati wa chakula cha jioni kilichoandaliwa na Kamati ya Amani ikiwa ni kusheherekea Sikukuu ya Krismasi.

Waziri huyo alisema bado kuna viashiria vya mtu mmoja mmoja na vikundi vya watu wanaotaka kuvuruga amani, vitendo ambavyo Serikali haitavivumilia.

Mwenyekiti wa Kamati ya Amani Mkoa wa Dar es Salaam, Alhadi Musa Salum alisema ni mara ya kwanza kwa Waislamu kualikwa na kukaa pamoja katika kusheherekea Sikukuu ya Krismasi.

“Pamoja na kuwapo kwa mahusiano mazuri kati ya Wakristo na Waislamu nchini bado kumekuwa na shida kwa baadhi ya watu pale tunapokaa pamoja katika sikukuu hizi na kushindwa kutofautisha kusherehekea na kutambua,” alisema.

Naye Askofu wa Kanisa la Ufufuo, Paul Bendera alisema siku zote amani inatoka kwenye moyo wa mtu. 

“Haiwezekani tunakakaa pamoja akatokea mtu akatugawa, ili kuendeleza amani iliyopo tunapaswa kuthamini viongozi wetu na kutii mamlaka zao.”

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post