Ripoti:WATOTO WAHUKUMIWA KUNYONGWA SUDAN KUSINI


Ripoti ya Shirika la Kutetea Haki za Binadamu Amnesty International imesema watoto ni miongoni mwa wafungwa wanaonyongwa nchini Sudan Kusini . 

Shirika hilo limesema watu saba - akiwamo mtoto mmoja - walinyongwa na serikali ya Sudan mwaka 2018 - ikiwa ni idadi kubwa ya mauaji nchini humo tokea kuasisiwa kwake mwaka 2011. 

Amnesty International limeeleza kwamba wafungwa wawili ambao walikuwa watoto walipohukumiwa walinyongwa mwaka jana. 

Ripoti hiyo imesema mtoto wa kiume wa miaka 16 ambae akiwa na miaka 15 alihukumiwa, pamoja na mwanamke mwenye mtoto mchanga kwa sasa wamehukumia adhabu ya kifo katika gereza la mjini Juba. 

Kwa miaka mingi Sudan Kusini ilitumbukia katika vita wa wenyewe kwa wenyewe hadi kulipofikiwa makubaliano ya amani hivi karibuni. Makundi ya waanmgambo nchini humo yalikuwa yakitumia maelfu ya watoto kama wanajeshi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527