VIJANA WA CHADEMA WATINGA GEREZANI KUMUONA MBOWE,MATIKO



Baraza la vijana chadema (Bavicha) wakiongozwa na mwenyekiti Patrick Olesosop na mwenezi Edward Simbeye wamefika katika gereza la Segerea kwa ajili ya kumwona mwenyekiti wa chama hicho Freeman Mbowe na Ester Matiko waliofutiwa dhamana.

Bavicha walifika Segerea majira ya saa nne ikiwa ni utekelezaji wa hadi yao ambayo waliitoa juzi Desemba 8 ambapo Mwenyekiti wao Patrick Ole Sosopi alisema kufuatia kuahirishwa kwa sherehe za Uhuru, wamepanga kutembelea magereza mbalimbali nchini ili kuzungumza na wafungwa na mahabusu.


Sosopi alisema wameamua kufanya hivyo baada ya Serikali kutangaza kuahirishwa kwa sherehe za miaka 57 ya Uhuru, ambapo fedha zilizokuwa zimetengwa kwa ajili ya shamrashamra hizo zitatumika kujengea Hospitali ya Uhuru jijini Dodoma.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527