Friday, November 2, 2018

KAULI YA ZITTO KABWE BAADA YA KUACHIWA KWA DHAMANA

  Malunde       Friday, November 2, 2018
Mbunge wa Kigoma Mjini na kiongozi wa Chama Cha ACT – Wazalendo, Zitto Kabwe amedai makosa anayoshtakiwa yanafanana na makosa ambayo walishawahi kushtakiwa baadhi ya waasisi wa bara la Afrika.

Kwa mujibu wa Zitto Kabwe, amedai kuwa kesi za namna hiyo ndizo zilizowahi kuwakumba baadhi ya waasisi, akiwemo muasisi wa Taifa la afrika kusini, Nelson Mandela pamoja na muasisi wa  Tanzania Mwalimu Julius Nyerere.

Akizungumza mara baada ya kupatiwa dhamana, Zitto Kabwe amesema ; “Kesi za namna hii wamefungwa wakina mandela, na mwalimu kwa hiyo sio jambo linalopaswa kuwatisha watu. Ila nasikitika sana jana sikushiriki kongamano la chuo kikuu cha Dar es salaam.

“Naamini lazima tuweze kutoa tafsiri mbadala juu ya kile kilichotokea jana, pia niwatake watanzania tuwe na mshikamano ili kuhakikisha nchi yetu inakuwa imara.”

Mbunge huyo wa Kigoma mjini anashtakiwa kwa makosa matatu ya uchochezi, ambapo katika kesi yake upande wa Jamhuri unawakilishwa na Wakili, Tumaini Kweka na upande mshtakiwa unawakilishwa na wakili Peter Kibatala.

Zitto alikamatwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es salaam oktoba 31 mwaka huu kufuatia mkutano wake na waandishi wa habari ambapo alitoa madai ya kuawawa kwa zaidi ya raia 100 katika Wilaya ya Uvinza Mkoani Kigoma.

Kesi ya Mbunge huyo inatarajiwa kuendelea tena Novemba 12 mwaka huu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post