UCHOMAJI WA MAITI WAZUA WASIWASI WA MIZIMU ZIMBABWE

Uchomaji wa maiti umeleta mjadala mkubwa nchini Zimbabwe, na kutaka mila na desturi pamoja na imani za kidini kuzingatiwa.

"Kwa kuwa tumeumbwa kwa mavumbi na mavumbini tutarejea'', mstari huu kutoka kwenye Biblia unaleta uzito kidogo kwa waumini wengi wa kikristo nchini Zimbabwe ambao wanapinga utaratibu wa kuchoma maiti.

Wanafikiri kwamba ni bora kuzika kawaida na wanahisi kwamba mwili utarejelea kwenye mavumbi kiasilia tu badala ya kuuharakisha kuurudisha mavumbini kwa kuuchoma.

Uchomaji wa maiti huwa unatumia joto linalokadiriwa kufika nyuzi joto 500 mpaka nyuzi joto 800.

Mjadala huo unaendelea kuchukua vichwa vya habari katika mji wa Bulawayo,ambao ni wapili kwa ukubwa nchini Zimbabwe na kwao ni lazima kwa maiti kuchomwa kwa wale ambao wanakufa wakiwa na miaka 25 kushuka chini.

Mapendekezo hayo yalikuja zaidi ya mwaka mmoja tangu halmashauri iliposema kwamba watoto wenye umri wa miaka 10 na walio chini ya hapo inabidi wachomwe ili kusaidia kuondoa changamoto inayowakabili watu wa mipango miji.

Ongezeko la watu katika maeneo ya miji nchini Zimbabwe unasababisha maeneo ya kuzika kukosekana.

Chanzo:BBC Swahili

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post