POLISI MWANZA WADAI KUUA MAJAMBAZI SABA | MALUNDE 1 BLOG

Friday, November 16, 2018

POLISI MWANZA WADAI KUUA MAJAMBAZI SABA

  Malunde       Friday, November 16, 2018
Kamanda wa Polisi Mkoa Mwanza, Jonathan Shana amethibitisha kuaa kwa watu 7 wanaosadikika kuwa ni majambazi, katika eneo la kishiri kwenye majibizano ya risasi na jeshi la polisi.

Kamanda Jonathan Shana amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia leo mtaa wa Ihushi kata ya Kishiri wakati jeshi la polisi likifanya doria maalum mkoani humo.

“Hilo tukio la Kishiri limetokea majira ya saa 4 usiku wa kuamkia leo, na majambazi wote wameuawa wakati wa mapigano ya kurushiana risasi na jeshi la polisi na katika mapigano hayo tumekamata silaha mbili za kivita na risasi zaidi ya 71, majambazi wote wameuawa.”

Kamanda Shana amesema kabla kutokea makabiliano ya kurushiana risasi, polisi walifanikiwa kumtia mbaroni mtuhumiwa mmoja ambaye ndiye aliwaongoza hadi kwenye maficho yao na kuwakurupusha wengine ambao badala ya kujisalimisha walianza mashambulizi ya risasi yaliyojibiwa na polisi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post