Breaking : ABDUL NONDO AIBWAGA SERIKALI MAHAKAMANI...KAACHIWA HURU


Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa imemuachia huru Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi (TSNP), Abdul Nondo leo Novemba 5 ,2018 baada ya kutomkuta na hatia dhidi ya makosa yake mawili aliyokuwa akishtakiwa.

Nondo alikuwa akikabiliwa na makosa mawili moja la kutoa taarifa za uongo kwa kudanganya kama alitekwa akiwa jijini Dar es salaam na baadaye kukutwa Mkoani Iringa.

Nondo alikuwa akitetewa na Wakili wa Jebra Kambole kwa kushirikiana na mawakili kutoka kituo cha Haki za binadamu na mtandao wake wanafunzi ambapo katika uamuzi huo mahakama ilimkuta Nondo hana hatia na kuamuru aachiwe huru.

Hivi karibuni Abdull Nondo ambaye alikuwa ni Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini aliandika barua ya kuomba kujiuzulu nafasi yake kutokana na sababu binafsi jambo ambalo lilikubaliwa na viongozi wa mtandao huo.

Aidha Nondo pia ni miongoni mwa watu ambao walikuwa wakichunguzwa uraia wao na mamlaka ya uhamiaji nchini ambapo alitakiwa kuambatanisha baadhi ya Nyaraka za wazazi wake.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post