MBOWE AMKINGIA KIFUA ZITTO KABWE KUNYIMWA DHAMANA

Sakata la kukamatwa kwa Mbunge wa Kigoma mjini (ACT-Wazalendo), Zitto Kabwe na kushindwa kupatiwa dhamana jana Oktoba 31, kumemuibua kiongozi wa kambi rasmi ya upinzani Bungeni Freeman Mbowe na kudai kuwa wabunge waupinzani waachwe wafanye kazi yao.

Mbowe ambaye pia ni mwenyekiti wa CHADEMA taifa, amefunguka hayo kupitia ukurasa wake wa kijamii wa twitter ambapo ameandika kuwa, "Mhe Zitto kasema na Vyombo vya Ulinzi na Usalama vimehusishwa. Wanasiasa wa Upinzani waachwe wafanye kazi yao, mtuhumiwa asiwe Hakimu. Serikali ijibu hoja kwa vielelezo, ikilazimu iunde tume huru za uchunguzi na CHADEMA tutasimama na ACT".


Zitto alikamatwa na polisi jana saa 5 asubuhi na kupelekwa kituo cha polisi Oysterbay ambako alihojiwa kwa takribani saa tatu, kisha kuhamishiwa kituo kikuu cha polisi ambapo Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Liberatus Sabas aliwaeleza wanahabari kuwa wanamshikilia Zitto kutokana na matamshi aliyoyatoa hivi karibuni kuhusiana na mauaji ya askari na raia wilayani Uvinza mkoani Kigoma.


Mpaka jana usiku kwa mujibu wa Wakili wake, Jebra Kambole, mwanasiasa huyo amenyimwa dhamana na Jeshi la Polisi ambalo limesema kuwa ataendelea kushikiliwa kwa ajili ya mahojiano zaidi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527