BOKO HARAM WASHAMBULIA VIJIJI VITATU, WAUA WATU 12

Wapiganaji wa kikundi cha kigaidi cha Boko Haram, wamevishambulia vijiji vitatu vya Bulaburin, Kofa na Dalori nje kidogo ya mji wa Maiduguri katika Jimbo la Borno na kusababisha maafa makubwa kwa wananchi.

Kwa mujibu wa Shirika la Habari la Al Jazeera, watu 12 wamefariki dunia katika tukio hilo baada ya Boko Haram kuvishambulia vijiji vitatu vilivyoko Kaskazini-Mashariki mwa Nigeria.

Mashuhuda wanasema wanamgambo wa Boko Haram wanadaiwa kuwasili wakiwa ndani ya magari saba na kuvishambulia vijiji vya Bulaburin, Kofa na Dalori nje kidogo ya mji wa Maiduguri katika Jimbo la Borno.

“Magaidi walifanya mashambulizi makubwa na kuchoma moto vijiji vya Bulaburin na Kofa baadaye wakaendelea hadi kijiji cha Dalori ambako nusu yake kimeshambuliwa na kuchomwa moto,” alisema shuhuda Babakura Kolo, alipozungumza na shirika la habari la AFP.

“Wameua watu tisa Kijiji cha Bulaburin, wawili katika Kijiji cha Dalori, lakini waliposhambulia Kijiji cha Kofa walipora vyakula na kuchoma moto

Takribani nyumba 10,000 zimechomwa moto katika Kijiji cha Dalori.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527