WATALII WALAZAMIKA KUONGEZA SIKU KATIKA HIFADHI YA TAIFA YA SERENGETI KUSHUHUDIA TUKIO LA KUHAMA KWA MAKUNDI YA NYUMBU WAKITOKEA KENYA.


Watalii wakiwa kando ya Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,eneo la Kogatende wakishuhudia tukio kubwa la kuhama kwa Makundi Makubwa ya Nyumbu wakivuka mto kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Kundi la Nyumbu likijiandaa kuvuka Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Nyumbu wakivuka Mto Mara kuingia katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti .
Baadhi ya Watalii wamelazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti kwa ajili ya kushuhudia tukio hilo la aina yake ambalo hutokea kila mwaka .
Kundi kubwa la Nyumbu likiwa katika maandalizi ya kuvuka Mto Mara kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Magari yaliyobeba Watalii yakiwa yameegeshwa kando ya Mto Mara kusubiri tukio la kuvuka kwa Makundi ya Nyumbu katika Mto Mara kuingia Hifadhi ya Taifa ya Serengeti.
Mamba wakiwa Mto Mara katika Hifadhi ya Taifa ya Serengeti wakiwa katika mawindo ya Mnyama Nyumbu wakati akivuka.
Mnyama Pundamlia wakiwa upande wa pili mwa Hifadhi ya Taifa ya Serengeti ,tunaweza sema ni kama wako hapo kwa ajili ya mapokezi ya Nyumbu wanarudi kutoka katika Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya.
Eneo la Mto Mara ambapo Watalii wakingojea tukio la kuvuka kwa Makundi ya Nyumbu.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii. 

Hifadhi ya Taifa ya Serengeti iliyopo Mkoani Mara,imeendelea kuwa maarufu Duniani na kuvutia watalii wengi zaidi kutoka maeneo mbalimbali ya Dunia kwa ajili ya kujionea tukio la kila mwaka la kuhama kwa Makundi makubwa ya Nyumbu kutoka Hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya na kuingia Serengeti. 

Tukio hili ambalo hutokea kuanzia mwezi Julai na wageni kulipa jina la “Great Wildebeest Migration” mwaka huu linatajwa kuvutia watalii wengi zaidi huku wengine wakilazimika kuongeza siku za kukaa katika Hifadhi ya Serengeti wakingojea kushuhudia tukio hilo. 

Mwandishi ameshuhudia Msururu wa Magari ya kubeba watalii yakiwa na wageni kando ya Mto Mara kusubiri kujionea hali inavyokuwa wakati wanyama hao wakivuka kwa makundi kutoka upande mmoja wao kuingia Hifadhi ya Serengeti. 


Eneo la Mto Mara ambapo Wanyama hawa wamekuwa wakivuka linatajwa kuwa na Vivuko 10 hali inayochangia waongoza watalii kufuata mwenendo wa Nyumbu kwa sababu si rahisi kufahamu wapi wataelekea kuvuka jambo ambalo hutumia zaidi ya saa 5 hadi 7 kungojea tukio hilo. 

Tukio la misafara ya makundi ya wanyama hao kuhama na kurudi hubadilika kila mwaka kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa na kiwango cha maji katika mto mara hata hivyo limeendelea kuwa kivutio kikubwa kwa wageni. 

Kivutio kikubwa katika misafara ya wanyama hao ambao wamekuwa wakiondoka nchini kila mwaka kuanzia mwezi mey na kurudi kuanzia mwezi julay ni namna wanavyovuka mto mara na jinsi wanavyokabiliana na wanyama wengine ndani ya mto huo wakiwemo Mamba

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527