Tanzia :PRODUCER PANCHO LATINO AFARIKI DUNIA......MASTAA,WADAU KILIO KONA


Mtayarishaji kutoka tasnia ya Bongo Fleva, Pancho Latino ambae alifanya kazi kwenye studio mbalimbali ikiwemo kwa Dully Sykes na Hermy B za B Hit’z amefariki jioni ya leo Jumanne Oktoba 9,2018 kwenye kisiwa cha Mbudya Dar es Salaam.

Chanzo cha kifo chake kimetajwa kwenye taarifa za awali kuwa ni kuzama kwenye maji kwenye kisiwa cha Mbudya.

Wadau mbalimbali wa sanaa na burudani wameanza kutoa pole kwa ndugu jamaa na marafiki kufuatia msiba huu mzito wa  producer Pancho Latino uliotokea leo October 9,2018 katika kisiwa cha Mbudya Dar es Salaam.

==>>Hawa ndio baadhi ya mastaa walioguswa na taarifa hizo na kuziandika kupitia kurasa zao za instagram

“Pancho Pancho Pancho nimeumia sana sina mfano wa maumivu niliyopata dah! Pumzika kwa Amani na Asante kwa mchango wako mkubwa katika Muziki Wetu…Bwana alitoa na Bwana Ametwaa jina lake lihimidiwe” -Joh Makini

“Eh Mungu … 😭 Rest Easy Young Legend. Thankyou for everything you taught me, you raised me #BHitz you will live forever in the music 🙏🏾. Poleni Sana kwa familia nzima ya #BHitz #LatinoMafia@hermyb pigo kubwa kwenye tasnia ya muziki.” -Vanessa Mdee

“Rest In Power Latino Mafia!!!! 😔 I am Sad!! -Bdozen

“Doh..Upumzike kwa amani @pancholatino ..kazi ya Mungu na safari yetu ni moja..nimesikitika mno” -Mwana FA

“Daaah!!! Upumzike kwa Amani, sidhani kama ulikuwa umemaliza ulichokuwa nacho kichwani. Mapema sana, ila kazi ya Mungu haina makosa #RIP“-Marcochali

“Kutokana na msiba uliotufika hivi punde wa kuondokewa na producer Genius PANCHO LATINO kutoka B’HITS…Hatutaweza kuachia VIDEO Yetu ya#USHINDITENA kwa Leo…SO SAD Kwa kweli R.I.P PANCHO LATINO #RIP#genius#mafia #weusii“-Lordeyesmweusi


Advertisement

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post