WAZIRI DKT. KIGWANGALLA, PROF. KABUDI WAUNGURUMA LONDON, MAPAMBANO YA BIASHARA HARAMU YA NYARA


Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mawaziri wake Waziri wa Maliasili na Utalii Dkt. Hamisi Kigwangalla na Waziri wa Katika na Sheria Profesa Palamagamba Kabudi wameweza kuhutubia mkutano mkubwa na wa Kimataifa juu ya upigaji vita biashara haramu ya nyara, uliokuwa wa siku mbili Oktoba 11 na 12, 2018, Jijini London, Uingereza. 

Mhe. Dkt. Hamisi Kigwangalla na Mhe. Prof. Palamagamba Kabudi wamuwakilisha Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika mkutano huo wa Kimataifa na kuandaliwa na Serikali ya Uingereza chini ya Uenyekiti wa Mjukuu wa Malkia wa Uingereza Prince William.

Mwaka huu mkutano huo ni wa Nne wa Ngazi ya juu kuhusu Biashara haramu ya nyara ambao huku ukiwakutanisha viongozi wakuu wa nchi, mawaziri na wataalam kutoka zaidi ya nchi 60 Duniani pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali, wasomi na wafanyabiashara.

Mkutano huo una lengo la kuimarisha jitahada zinazofanywa na Serikali mbalimbali duniani katika kupambana na kuzuia biashara haramu ya nyara.

Mawaziri hao wa Tanzania kwa nyakati tofauti wameweza kusoma hotuba zao zenye malengo ya na jitihada za Serikali ya Tanzania katika uhifadhi wa Maliasili na kupambana na biashara haramu ya nyara hususani katika hifadhi zake za taifa na maeneo yote ya mapori ya hakiba sambamba na shoroba zilizopo.

Imeelezwa kuwa, Tanzania ni moja ya nchi ambayo imetenga asilimia 32.5% ya eneo lake kwa ajili ya uhifadhi na inasifika kwa uwingi wa bayoanuai.

Jitiada za kuzuia ujangili zimepelekea kupungua kwa ujangili kwa asilimia 50 na hii imejidhihirisha kwa kuongezeka kwa Tembo kutoka 43330 mwaka 2014 hadi kufikia tembo 59830 mwaka 2015. Kwa zaidi ya Asilimia 60.

Wakati akizungumza katika mkutano huo, Mwenyekiti wa Mkutano huo Prince William wa Uingereza alisifu jitihada zinazofanywa na Serikali ya Tanzania katika uhifadhi na upambanaji wa Biashara haramu ya nyara. 

Prince William alipongeza jitihada alizozishuhudia wakati wa ziara yake nchini Tanzania zikiwemo kutoka Elimu ya uhifadhi kwa wanafunzi pamoja na vyuo vizuri vya Elimu ya uhifadhi kikiwemo Chuo cha Elimu ya Uhifadhi wa Wanyamapori Mweka.

Madhumuni ya mkutano huo ni kujenga ushirikiano baina ya nchi, taasisi binafsi na za kiserikali, NGOs na Wanataaluma, pia unalengo la kubadilishana uzoefu na mbinu za kupunguza mahitaji ya soko la nyara kwa nia ya kulifunga soko hilo duniani.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527