Picha : MBUNGE AZZA HILAL AMWAGA VIFAA TIBA VYA MILIONI 36.5 KWENYE VITUO VYA AFYA WILAYANI KAHAMA

Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) amekabidhi msaada wa Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati sita zilizopo katika halmashauri ya wilaya ya Ushetu,Msalala na Kahama Mji wilayani Kahama mkoani Shinyanga.

Mheshimiwa Azza amekabidhi vifaa tiba hivyo leo Jumanne Oktoba 16,2018 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kahama,Anamringi Macha wakati wa Kikao cha Baraza la UWT wilaya ya Kahama kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.

Vifaa tiba hivyo ni pamoja na shuka 100,mashine za kupima damu,wingi wa damu,sukari,joto,mapigo ya moyo na vifaa vya kusaidia kujifungua kwa akina mama ambavyo kupatikana kwake kumetokana na jitihada za mbunge huyo kuhakikisha vifo vya mama na mtoto vinapungua mkoani Shinyanga.

Awali akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa tiba hivyo,Mheshimiwa Azza Hilal alisema kupitia Kampeni yake ya ‘Afya Yangu Mtaji Wangu’ na kuwajali akina mama aliamua kutafuta wadau kwa ajili ya kusaidia kumaliza changamoto ya uhaba wa vifaa tiba katika vituo vya afya na zahanati.

“Nawashukuru sana Bahari Pharmacy Ltd na Brett &Beileys kwa kunishika mkono na kuchangia kupatikana kwa vifaa hivi ambavyo leo navikabidhi ili vikatumike kwenye zahanati na vituo vya afya kwani hatutaki kuona vifo vya mama na mtoto”,alieleza Azza.

“Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Jemedari,Dkt. John Pombe Magufuli imedhamiria kuboresha huduma za afya,na tutaendelea kushirikana ili kuhakikisha wananchi wanakuwa na afya bora ili washikiriki katika shughuli za uchumi”,aliongeza.

Alivitaja vituo vya afya vitakavyonufaika na msaada huo kuwa ni Mwendakulima,Mbika na Lunguya na zanahati ambazo ni Ngogwe,Kisuke na Bulige.

Akipokea vifaa tiba,Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha alimshukuru mbunge huyo kwa msaada huo na kubainisha kuwa ameunga mkono kwa vitendo ilani ya CCM na juhudi zinazofanywa na Rais Magufuli katika kuboresha sekta ya afya.

“Nikupongeze sana kwani umetumia cheo chako kwa faida ya wote badala ya kujinufaisha wewe mwenyewe,lakini nikushukuru pia kwa kuendelea kujitoa kwa hali na mali katika kukitumikia chama na wananchi,umekuwa kiungo mzuri sana”,alisema Macha.

Kwa Upande wake Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi aliahidi kumuunga mkono mheshimiwa Azza kwa kutoa msaada wa vifaa tiba katika vituo vitatu vya afya wilayani Kahama.

ANGALIA PICHA ZA MATUKIO HAPA CHINI
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) akizungumza wakati akikabidhi vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama leo katika ukumbi wa Halmashauri ya Mji Kahama.Kushoto ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria,kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga.  - Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog
Vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 36.5 kwa ajili ya zanahati na vituo vya afya wilayani Kahama vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad (CCM) kwa kushirikiana na wadau wake Bahari Pharmacy Ltd na Brett &Beileys.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha(aliyevaa miwani) akiangalia vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad.
Kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akimshukuru Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad kwa kuleta vifaa tiba wilayani Kahama. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi. 
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi vifaa tiba kwa  Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akikabidhi shuka ikiwa ni sehemu ya shuka 100 alizotoa kwa ajili ya vituo vya afya na zahanati wilayani Kahama.
Wa pili kulia ni Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akiwa ameshikilia boksi lenye mashine ya kupimia sukari mwilini. Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kahama Thomas Myonga.Wa kwanza kushoto ni  Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akifuatiwa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa ameshikiliwa vifaa tiba.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya Ushetu,Dk. Joseph Mugizi akisoma maandishi katika mashine/kifaa cha kupimia sukari baada ya kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Kahama,Anamringi Macha.
Kushoto ni Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kahama,Dk.  David Lucas akipokea mashine/kifaa cha kupimia wingi wa damu.
Mwakilishi wa Mganga mkuu wa Halmashauri ya wilaya Msalala,Dk. Martine Dotto akipokea kifaa cha kupimia mapigo ya moyo.
Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Mji Kahama,Dk.  David Lucas akiwa ameshikilia kifaa cha vifaa vya kujifungulia kwa akina mama.Katikati ni Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akifafanua kuhusu vifaa vya kujifungulia.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa UWT halmashauri ya wilaya ya Ushetu
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa UWT halmashauri ya wilaya ya Kahama Mji.
Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe wa UWT halmashauri ya wilaya ya Msalala.
Mkuu wa wilaya ya Kahama Anamringi Macha akizungumza baada ya kupokea vifaa tiba vilivyotolewa na Mbunge wa Viti Maalum mkoa wa Shinyanga Mheshimiwa Azza Hilal Hamad.Wa kwanza kulia ni Mwenyekiti wa UWT wilaya ya Kahama,Telephora Saria.
Mbunge wa Jimbo la Ushetu,Mheshimiwa Elias Kwandikwa ambaye ni Naibu Waziri wa Ujenzi akizungumza wakati Mheshimiwa Azza Hilal akikabidhi vifaa tiba.
Picha zote na Kadama Malunde - Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527