MAMA AMCHOMA MOTO MWANAE

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi Kinondoni Muliro Jumanne Muliro amethibitisha kukamatwa kwa mwanamke anayetuhumiwa kumuunguza mtoto wake wa kumzaa kwa mafuta ya taa kwa madai ya kuiba kiasi cha shilingi laki mbili zilizokuwa zimehifadhiwa ndani.


Kamanda Muliro amesema mtoto aliyefanyiwa ukatili huo ni wa kike ambaye anasoma kidato cha kwanza shule ya Sekondari Magomeni na alifanyiwa hivyo usiku wa kuamkia Septemba 1, 2018 maeneo ya Boko Magereza.


''Hili ni kosa la jinai na alikusudia huwezi kusema ni bahati mbaya wakati mtu amenunua mafuta na amefanya maandalizi kabisa, kwahiyo sisi kama chombo cha dola kazi yetu ni kuhakikisha tunamfikisha katika mkono wa sheria kwa ukatili aliomfanyia mtoto wake mwenyewe'', amesema.


Kamanda Muliro ameweka wazi kuwa mtuhumiwa atafikishwa mahakamani muda wowote kuanzia sasa kwakua taratibu za kipolisi zimekamilika.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post