CBA YATOA MSAADA WA MILIONI 4 SHULE YA SINGISI


Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani Akikabidhi hundi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Singisi ,Safira Ndelwa.Benki hiyo imetoa msaada huo kwa ajili ya mabati na ukarabati wa madarasa.Picha na Pamela Mollel,Arusha 
Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani Akikabidhi hundi ya shilingi milioni 4 kwa Mkuu wa Shule ya Msingi Singisi ,Safira Ndelwa.Benki hiyo imetoa msaada huo kwa ajili ya mabati na ukarabati wa madarasa 
Mkuu w Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani akizungumza katika hafla ya kukabidhi hundi ya milioni 4 kwa ajili ya kusaidia shule ya msingi Singisi.
Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani akikabidhi hundi kwa mwanafunzi wa shule ya msingi Singisi
Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano benki ya CBA,Julius Konyani akipokea zawadi kutoka wanafunzi wa shule ya msingi Singisi.
Picha ya pamoja


Na Pamela Mollel,Arusha.


Benki ya CBA  imetoa msaada wa shilingi milioni 4 kwa shule ya msingi Singisi kwa ajili ya mabati pamoja na ukarabati wa shule hiyo ili kusaidia kutatua changamoto ya uhaba wa madarasa na uchakavu wa majengo.

Mkuu wa Idara ya wateja ,masoko na mawasiliano,Julius Konyani alisema wameamua kutoa msaada huo ili kusaidia watoto wa kitanzania waweze kupata elimu bora ambayo itawasaidia kujikwamua kiuchumi na kuondokana na umaskini.

Julius alisema  benki hiyo imeamua kurudisha sehemu ya faida kwa wananchi kwa kutoa fedha hizo licha ya msaada huo wamekua wakisaidia chumba cha watoto njiti kwa kutoa vifaa vya kitaalamu ili kuokoa maisha ya watoto.

Mkuu wa Shule hiyo Safira Ndelwa ameshukuru msaada huo ambapo alisema msaada huo utawasaidia kumalizia ujenzi wa uzio wa shule hiyo pamoja na kukarabati majengo ya shule hiyo ambayo ni chakavu.

Hata hivyo aliiomba benki hiyo iwasaidie kuwajengea vyumba vya madarasa kwani shule hiyo inakabiliwa na uhaba wa madarasa hali inayosababisha msongamano darasani inayowalazimu kuingia darasani kwa awamu huku walimu wakifundisha kwa zamu.

“Tunaomba benki ya CBA isituache iendelee kutusaidia katika maeneo mengine ambayo kuna changamoto ili wanafunzi waweze kusoma katika hali bora”,alisema. 

Diwani wa Kata ya Seela Singisi Penzila Palangyo alisema ushiriki wa sekta binafsi katika maendeleo ya elimu ni muhimu ili kuhakikisha kuwa sekta ya elimu inasonga mbele na kusaidia maisha ya watu wengi.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527