Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BUNDI ATUA STAND UNITED ...KATIBU MKUU,MJUMBE WA KAMATI TENDAJI WAJIUZULU

Jackline Isaro

Taarifa tulizopata mchana huu zinasema Katibu Mkuu wa Timu ya Stand United Kennedy Nyangi na Mjumbe wa kamati tendaji wa timu ya Stand United 'Chama la Wana' ya Shinyanga Jackline Isaro wameandika barua za kujiuzulu nafasi zao kuanzia leo Agosti 18,2018.


Katika barua yake kuhusu uamuzi huo amesema chanzo cha uamuzi wa kujiuzulu nafasi hiyo ni kutokana na kutoelewana na viongozi wake akidai wamekuwa wakifanya mambo yasiyoendana na katiba ya Stand United.

"Sababu ya uamuzi huu wa kujiuzulu ni kutoelewana na viongozi wangu kwa kufanya mambo yasiyoendana na katiba,nikihoji ndipo lawama na kelele zinaanza kuniandama" - Isaro.
Wakati Isaro akijiuzulu,Katibu Mkuu wa Stand United Kennedy Nyangi naye ameandika barua ya kujiuzulu.

"Nimeshindwa kuendelea kutumikia klabu katika nafasi ya katibu mkuu",sehemu ya maandishi yanayoonekana katika barua inayosambaa mtandaoni ikidaiwa kuandikwa na Kennedy Nyangi.


Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com