DC JOKATE : NIDHAMU,BIDII,USHIRIKIANO VITAIJENGA KISARAWE

Ikiwa ni kwa mara ya kwanza katika historia, Mkuu wa wilaya mpya wa Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo amekutana na watumishi wa wilaya ya Kisarawe kwa lengo la kutambulishana ,kufahamiana na kuweka mikakati jinsi ya kuwahudumia wananchi katika kuleta maendeleo yao na wilaya kwa ujumla.


Kikao hicho kimefanyika Agosti 6,2018 kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe.

Awali akimkaribisha mkuu wa wilaya ili azungumze na watumishi ,Katibu Tawala wa wilaya ya Kisarawe,Mtela Mwampamba aliwatambulisha watumishi hao mbele ya Mkuu wa Wilaya kwa kutambulisha watumishi hao kwa kila idara na vitengo na kueleza kwa kifupi matarajio ya watumishi kwa ujio wa mkuu wa wilaya mpya.

Akizungumza katika kikao hicho, Mheshimiwa Jokate Mwegelo alisema  ili kuwaletea maendeleo wananchi panatakiwa kuwepo ushirikiano katika utekelezaji wa majukumu katika kuwahudumia wananchi wa Kisarawe na kuwaletea maendeleo kama ilivyoainishwa kwenye utekelezaji wa mipango ya serikali inayOtekeleza ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015-2020.

"Lengo kuu la kukuatana hapa ni kufahamiana na kuwekana sawa naamini tutakuwa watumishi wa mfano bora na wa kuigwa,ili tusonge mbele tunahitaji kuwa na nidhamu ya kazi, bidii na ushirikiano’’ ,alisema.

Kaimu mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Kisarawe Patric Allute alisema watatekeleza maagizo yote ili  kuwahudumia na kuwaletea maendeleo wananchi.
Mkuu wa Wilaya mpya wa Kisarawe Mheshimiwa Jokate Mwegelo akizungumz na na watumishi wa wilaya ya Kisarawe 



Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527