Msanii wa Bongo Fleva, Harmonize tayari ameingia location kwa ajili ya kufanya video ya wimbo aliofanya na Professor Jay.
Muimbaji huyo kutokea lebo ya WCB ame-share video kupitia Insta Stori wakiwa locationi maeneo ya Kariakoo Dar es Salaam, director wa video hiyo ni Kenny ambaye pia amehusika katika video ya wimbo Kwangwaru ambayo Harmonize amemshirikisha Diamond.
Wimbo wa Harmonize na Professor Jay unakwenda kwa jina la Atarudi akiwa umetengenezwa na producer Bonga. Tayari Harmonize ameweka wazi kuwa wimbo huo utatoka August 28, 2018.
Social Plugin