DC MURO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA

Mkuu wa wilaya ya Arumeru Mh.Jerry Muro amefanya ziara ya kushtukiza  katika baranara ya mchepuko Arusha Bypass katika eneo la muungano Makumira  na kubaini uwepo wavitendo vinavyoashiria ukiukwaji wa taratibu za kazi na haswa katika kazi zinazofanywa na  raia  kutoka nje.

Mh Muro Pamoja nakuridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa barabara hiyo itakayosaidaia kupunguza msongamao wa magari kuelekea Jijini Arusha ameonyeshwa kukerwa na tabia ya baadhi ya wageni kufanya kazi zinazoweza kufanywa na watanzania jambo linaloendela kuminya fursa ya vijana wa kitanzaia kupata ajira.

Kutokana na sababu hiyo DC Muro alilazimika kuchukua hatua  ya kuwaagiza maofisa wa Uhamiaji kufuatilia suala hilo jambo lililopelekea kubainika uwepo wa raia tisa ( 9 ) wa kigeni wanaofanya kazi hizo pasipo kuwepo na baadhi ya vibali husika vya kufanya kazi.

Katika ziara hiyo DC Muro aliambatana na Naibu katibu Mkuu wa Jumuiya ya Afrika Mashariki Mhandisi Steven Mlote ambao ni waratibu wa ujenzi wa Barabara hiyo.

DC muro anaendelea na zoezi la ukaguzi wa miradi mbalimbali ya ujenzi katikaa wilaya ya Arumeru yenye kata 53 na Halmashauri mbili za Arusha Dc na Meru Dc.

Imetolewa na Ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Arumeru

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527