Tuesday, July 17, 2018

STAND UNITED YAZITISHIA NYAU KLABU KONGWE..YASAJILI VICHWA KUTOKA BURUNDI

  Malunde       Tuesday, July 17, 2018

Mwenyekiti wa Stand United Dkt. Ellyson Maeja akizungumza na waandishi wa habari leo mjini Shinyanga.

Timu ya Stand United Chama la Wana ya Mjini Shinyanga imezitishia nyau klabu kongwe nchini kwa kufanya usajili wa wachezaji wawili wataalamu wa kuchungulia nyavu kutoka nchini Burundi.

Akizungumza na waandishi wa habari leo Jumanne Julai 17,2018, Mwenyekiti wa Stand United Dkt. Ellyson Maeja amesema wamepata saini za wachezaji ambao wataisaidia Stand United kupata matokeo chanya.

Dkt. Maeja amewataja wachezaji hao kuwa ni Alex Kitenge mshambuliaji,Hafeez Musa wote kutoka timu ya Lydia ya nchini Burundi.

Amesema wachezaji ambao wameachwa huru kujiunga na vilabu vingine ni Hamad Kibopile,Salvatory Nkulila,John Mwenda,Kisatya Sahani,Kitoba Emmanuel,John Lwitiko,Rajabu Rashid na Ally Mabrouk.

Dkt. Maeja ameunga mkono hatua ya Shirikisho la Mpira wa Miguu nchini (TFF)kuruhusu timu kufanya usajili kwa wachezaji 10 wa nje na kusema kwamba hiyo ni changamoto kwa vijana wa Kitanzania kutumia fursa kujitangaza kisoka.

Aidha mbali na kumpongeza mdhamini wao Jambo Food Products Co. Ltd, Dkt. Maeja amesema wamekuwa na mazungumzo na Kampuni ya Kahama Oil Mills ili kuisaidia kwa baadhi ya mahitaji hasa pesa ya uendeshaji.

Na Malaki Philipo – Malunde1 blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post