Monday, July 2, 2018

RAIS MAGUFULI AFUNGUKA ANAVYOKERWA MADUDU UONGOZI WA JUU WIZARA YA MAMBO YA NDANI

  Malunde       Monday, July 2, 2018

Rais John Magufuli amesema hajapendezwa na utendaji kazi wa uongozi wa juu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kutokana na wizara hiyo kufanya mambo ya ovyo.


Ametoa kauli hiyo leo Jumatatu Julai 2, 2018 Ikulu Dar es Salaam, muda mfupi baada ya kuwaapisha viongozi aliowateua akiwemo Waziri wa Wizara hiyo, Kangi Lugola ambaye kabla ya uteuzi huo alikuwa Naibu Waziri Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Amesema ukiondoa kazi zinazofanywa na makamishna, hajapendezwa na utendaji wa uongozi wa juu.

“Nakupeleka pale ukafanye kazi na wewe bahati nzuri ni askari. Nilifanya uchunguzi wa miradi ya polisi katika vituo 108, palikuwa na mkataba wa Wizara ya Mambo ya Ndani pamoja na mtu anaitwa Lugumi wa Sh37bilioni,” amesema.


“Tulipewa maagizo kama Serikali tuyashughulikie na tuyatafutie ufumbuzi lakini mpaka leo hii haijapatiwa ufumbuzi,”.

Na Asna Kaniki, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post