PUNDA APAKWA RANGI AFANANE NA PUNDAMILIA

Bustani ya wanyama nchini Misri imekana kumpaka rangi punda ili kumfanya afanane na pundamilia baada ya picha ya mnyama huyo kuonekana katika mitandao.

Mwanafunzi Mahmoud Sarhan aliweka picha hizo katika mtandao wa Facebook baada ya kuitembelea bustani ya wanyama mjini Cairo - International Garden municipal park.

Kando na kwamba mnyama huyo alikuwa mdogo, na masikio yake marefu kusimama wima, alionekana pia kuwa na rangi iliyotapakaa usoni mwake.

Picha hizo zilisambaa kwa kasi huku wataalamu wakijadili kuhusu kizazi cha mnyama huyo.

Dakatri mmoja wa mifugo aliyehojiwa na kituo cha televisheni katika eneo hiloamesema kwamba pua ya pundamilia ni nyeusi , huku mistari yake ikiwa imefuatana na iko sambamba.

Sarhan ameiambia Extranews kwamba aliwapata wanyama wawili katika sehemu hiyo na wote walikuwa wamepakwa rangi.Pua ya Pundamilia ni nyeusi na masikio madogo kuliko punda wa kawaida


Hii sio mara ya kwanza kwa wasimamizi wa bustani kushutumiwa kujaribu kuhadaa umma.

Baada ya kushindwa kupata njia ya kuvuka kizuizi cha Israeli bustani moja ya wanyama huko Gaza iliwapaka rangi punda wawili ili wafanane kama pundamilia mnamo 2009.

Mnamo 2013 Bustani moja ya wanyama China katika jimbo la Guangxi ilishutumiwa kwa kuweka popo wa plastiki.
Chanzo- BBC
Theme images by rion819. Powered by Blogger.