Utafiti : ULAJI WA NJUGU UNABORESHA MBEGU ZA KIUME

Mabadiliko ya mtindo wa maisha hasa ulaji wa chakula bora huondoa matatizo ya uzazi kwa wanaume.


Ulaji wa njugu mara kwa mara kunaweza kuboresha afya ya mbegu za kiume.Utafiti umeeleza.

Wanaume waliokula njugu za lozi (almond),Hazeli(hazelnuts) na Jozi(walnuts) kwa kiasi cha kujaza kiganja cha mkono kila siku kwa siku 14 wanaweza kuimarisha mbegu zao za kiume kuwa nyingi na zenye kufanya kazi vizuri.Wanasayansi wamebaini.

Utafiti huu umekuja baada ya kuwepo kwa tatizo la ufanisi wa mbegu za kiume katika nchi za magharibi, tatizo linalosababishwa na uchafuzi wa mazingira, uvutaji sigara na aina za vyakula

Watafiti wamesema kuna ushahidi kuwa ulaji wa chakula bora unaweza kusaidia masuala ya uzazi.

Takriban pea moja ya wenza kati ya saba inakabiliwa na ugumu katika kushika mimba na takriban asilimia 40-50 ya tatizo hilo linatokana na wanaume.

Wanasayansi waliwagawa wanaume 119 kwenye makundi mawili ya umri wa kati ya miaka 18 na 35:

Kundi moja lilikula gramu 60 za njugu kwa siku kwenye mlo wao kundi jingine halikula njuguUvutaji wa sigara, matumizi ya pombe na uchafuzi wa mazingira ni miongoni mwa mambo yanayoathiri afya ya uzazi

Wale waliokula njugu walikuwa na mabadiliko kwenye mbegu zao:

Uzalishaji wa mbegu uliongezeka kwa 14%

Nguvu kwa ongezeko la 4%

Mwendo ongezeko kwa 6%

Umbo kwa 1%

Matokeo haya yanashuhudia kuwa mabadiliko kwenye mtindo wa maisha kama vile ulaji wa chakula bora ni faida.

Hatahivyo, watafiti wamefafanua kuwa wanaume waliotumika kwenye utafiti huu wote hawana tatizo la uzazi, hivyo haikuwa wazi kama matokeo ya utafiti yanaweza kutumika hata kwa wenye matatizo ya uzazi.

Chanzo- BBC

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527