Friday, July 13, 2018

HII HAPA ORODHA YA WANAFUNZI VINARA,SHULE BORA MATOKEO KIDATO CHA SITA 2018...NANE WAMEFUTIWA MATOKEO

  Malunde       Friday, July 13, 2018

Baraza la Taifa la Mitihani (Necta) limetangaza matokeo ya kidato cha sita leo Julai 13,2018 na kutoa orodha ya watahiniwa waliofanya vizuri zaidi kitaifa katika mtihani huo.

Katibu Mtendaji wa Necta, Charles Msonde, ametangaza matokeo hayo akiwa visiwani Zanzibar leo.


Watahiniwa waliofanya vizuri zaidi kitaifa katika masomo ya Sayansi ni pamoja na Anthony Mulukozi, wa Shule ya Sekondari ya Mzumbe, Asia Jasho wa Tabora Girls, na Raphael Fanuel wa Ahmes, Pwani.

Wengine waliofanya vizuri ni pamoja na Godfrey Kawau, Uru Seminari, Kilimanjaro na Biubwa Hamis Ussi, wa shule ya Sekondari ya Sos Hermain Gmeiner, Mjini Magahribi (Zanzibar).

Wengine ni Fahad Rashid Salum, shule ya Sekondari Lumumba, Mjini Magharibi, Prince Walter Ngao, Marian Boys, Pwani, Victor Maghembe, Marian Boys, Pwani na Emmy Shemdangiwa, St Marys Mazinde Juu, Tanga na Vanessa Lodrick Shoo wa St Marys, Mazinde Juu.


Baraza la Mtihani la Tanzania (NECTA) pia limezuia matokeo ya watahiniwa kumi na tatu kutokana na sababu kadhaa na wengine nane kufutiwa kabisa matokeo kwa sababu ya udanganyifu.

Akitaja sababu za kuzuiwa kwa matokeo hayo, Dkt. Msonde amesema kuwa kuna baadhi ya watahiniwa walishindwa kukamilisha mitihani yao kutokana na sababu za kiafya na hivyo kufanya mitihani nusu, watapewa nafasi ya kurudia mwaka unaofuata.

Licha ya hiyo, Dkt. Msonde amesema kuwa ufaulu umeongezeka kutoka asilimia 96.06% mwaka 2017 hadi 97.12% mwaka huu, huku ufaulu katika masomo ya sayansi umeshuka ukilinganishwa na masomo ya sanaa na biashara.

“Jumla ya watahiniwa 83,581 sawa na asilimia 97.58 ya watahiniwa waliofanya mitihani ya kidato cha sita Mei mwaka huu wamefaulu huku wasichana wakiwa ni 34,358, na wavulana waliofaulu ni 49,223 pekee”, amesema Dkt. Msonde.

Dkt. Msonde ameongeza kuwa tathmini ya hali ya matokeo imeonesha kuimarika kwa ufaulu katika madaraja ya I,II na III ikiwemo kupanda kwa asilimia 1.80 kutoka 93.72 mwaka 2017 na kuwa asilimia 95.52 mwaka 2018.

Shule zilizofanya vizuri zimetajwa kuwa ni Kibaha, Kisimiri, Kemebos na Mzumbe, Feza Boys, Marian Boys, AHMES, St Mary's Mazinde Juu, Marian Girls & Feza Girls.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post