HATIMAYE MWILI WA PATRICK WAWASILI DAR..KUZIKWA MAKABURI YA KINONDONI


Picha ya jeneza lililohifadhi mwili wa mtoto Patrick Peter.

Mwili wa mtoto wa muigizaji wa filamu nchini, Muna love, Patrick Peter, umewasili nchini leo saa 11:45 jioni na kupelekwa hospitali ya Aga Khan kwa ajili ya kuhifadhiwa.

Taarifa zilizotolewa na Baba Mdogo wa Marehemu, Patrick ambaye ndiye Mwenyekiti wa Kamati ya Mazishi amesema kwamba Mwili huo uliondoka Kenya saa 9:40 alasiri.

"Ratiba ya mazishi iko vilevile, kesho mwili utakuja nyumbani kwa baba wa mtoto Mwananyamala kwa ajili ya kuagwa na baadae utaagwa viwanja vya Leaders na utazikwa makaburi ya Kinondoni.

 "Tunashukuru mwili umeshawasili, na tayari tumeshaupeleka Aga Khan kwa ajili ya kuhifadhiwa. "amesema Bazo.

Bazo amesema, baada mwili huo kuwasili ratiba zitaendelea kama zilivyopangwa hapo awali.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527