CHILUNDA : FARIDI MUSSA AMENISHAWISHI


Shaban Idd Chilunda akishangilia goli katika mchezo wa ligi kuu dhidi ya Yanga.

Mshambuliaji chipukizi wa Azam Fc ambaye anatarajia kujiunga na klabu ya Tenerife ya Hispania, Shaban Idd Chilunda amefunguka na kusema kuwa ushawishi wa mchezaji, Farid Mussa anayechezea timu hiyo umemfanya aamue kujiunga nao.

Chilunda mwenye umri wa miaka 19, ameisaidia klabu yake ya Azam Fc kushinda kombe la CECAFA la Kagame mwaka huu kwa kuifunga Simba 2-1 katika mchezo wa fainali ambao aliifungia timu yake goli la kwanza.

Akizungumza na www.eatv.tv , Shaban Chilunda amesema.

"Kuhusu mazungungumzo kati yangu na Farid yalianza tangu akiwa anachezea hapa Tanzania, yeye ndiye amenifanya kwa namna moja ama nyingine nishawishike kujiunga na klabu ya Tenerife kwasababu ni mzoefu kwa sasa kule na atanisaidia kwa vitu vingi". 

Pia Shaban Chilunda amezungumzia kuhusu mkataba wake na klabu hiyo mpya na siku atakayoondoka nchini kuelekea Hispania, amesema.

"Mkataba wangu na Tenerife ni wa miaka miwili lakini kuna kipengele cha kuniuza kwa klabu yoyote itakayonihitaji, na kuhusu suala la kuondoka kwenda Hispania nasubiri muda wowote kibali cha kazi kikishafika nitaondoka". 

Shaban Idd Chilunda anatajwa kuwa miongoni mwa kipaji bora zaidi ambacho kitakuja kuisaidia timu ya taifa miaka mingi ijayo kwa uwezo wake wa kufumania nyavu, ambapo katika michuano ya Kagame pekee aliweza kufunga magoli nane yakiwemo manne katika mchezo wa nusu fainali dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda.
Chanzo- EATV

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527