Breaking : AJALI YAUA TENA MBEYA...MAGARI MATATU YAGONGANAWatu watano wanadaiwa kufariki dunia  katika ajali iliyohusisha lori pamoja na gari dogo aina ya Noah eneo la mteremko wa mlima Igawilo nje kidogo ya jiji la Mbeya usiku wa Alhamis Julai 5,2018 .

Ajali hiyo iliyohusisha magari matatu imetokea kwenye mteremko wa mlima Igawilo na kwa mujibu wa mashuhuda gari lenye kontena ililiangukia gari aina ya Noah iliyokuwa na abiria na inasadikiwa watu watano wamepoteza maisha.

Ajali hii imetokea ikiwa ni muda mfupi tu baada ya Waziri Mpya wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola kutembelea Mbeya na kutangaza kuvunja Baraza la Taifa la Usalama Barabarani pamoja na Kamati zake zote za Mikoa na WilayaTheme images by rion819. Powered by Blogger.