WANAOTANGAZA DAWA YA KUONGEZA MAUMBILE WASAKWA

MAMLAKA ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA), imeanza uchunguzi kusaka watu waliosambaza picha ya dawa maalumu ya wanyama, wakihamasisha watu kuitumia ili kuongeza maumbile mbalimbali ya miili yao.


Akizungumza na MTANZANIA kwa simu jana, Mkurugenzi wa Dawa na Bidhaa za Nyongeza wa TFDA, Adam Fimbo, alisema kitendo hicho ni kosa kisheria.

“Tunalifahamu hilo, tunachunguza, ni suala la matumizi ya mtandao, wanasambaza kwa watu wengi, madhara ya kuongeza mwili hasa kwa madawa yapo mengi mno,” alisema.

Alisema hata hivyo, madhara hayo hutegemea na aina ya kemikali zilizowekwa ndani ya dawa hizo.

“Hii iliyosambazwa mtandaoni ni ya vitamini, ingawa vitamini kiuhalisia haina madhara, lakini katika dawa hii imewekwa maalumu kwa matumizi ya wanyama na si binadamu,” alisema.

Fimbo alisema madhara mengine ya kuongeza mwili ambayo mhusika huyapata, ni ongezeko la mwili kupitiliza na kupata magonjwa yasiyo ya kuambukiza.

“Anakuwa kwenye hatari ya kupata shinikizo la damu, kisukari, moyo na mengine mengi,” alisema.

MTANZANIA lilianza kufuatilia habari hii kufuatia taarifa zinazosambazwa mitandaoni, zikionyesha dawa iitwayo Advit DE+H, inayoongeza …..

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527