Monday, May 28, 2018

TUNDU LISSU AFUNGUKA KURUDI TANZANIA

  Malunde       Monday, May 28, 2018

Mbunge wa Singida Mashariki, Tundu Antiphas Lissu amefunguka kwamba atarudi nchini siku atakayopona kwani Ulaya siyo kwao na kwa umri alionao hataweza kujifunza namna ya kuishi katika nchi za huko.

Lissu ameyasema hayo kupitia video fupi iliyorekodiwa na Mtanzaia Damian aishiye Uholanzi ambaye alikwenda kumuona katika hospitali aliyolazwa huko nchini Ubelgiji.

Lissu ameeleza kuwa kwa sasa anachosubiri ni kufanyiwa oparesheni moja itakayofanywa mwezi ujao na baadae ataanza matibabu ya kufanya mazoezi ya viungo na baada ya matibabu hayo yote wataweza kurejea nchini.

Lissu amesema kuwa ni lazima atarudi nchini Tanzania kwa kuwa umri alionao kwa sasa siyo umri wa kuanza kujifunza namna ya kuishi katika nchi hizo za ulaya ikiwa ni pamoja na kuhangaika kutafuta kazi.

Mbali na hayo Mbunge huyo ametoa ahadi kwa watanzania kuwa hatakuwa na cha kuwalipa pindi atakaporudi Tanzania bali atajitahidi kwa kadri yoyote ili kuhakikisha anatoa uwakilishi unastahili watanzania.

Lissu amesema kuwa baada ya serikali pamoja na Bunge kumtelekeza watanzania kwa umoja wao walihakikisha wanapambana kumuombea ikiwa ni pamoja na kutoa michango mbalimbali iliyomuwezesha yeye kupatiwa matibabu tangu akiwa hajitambui mpaka hatua ya sasa aliyofikia ambayo amebakiza oparesheni moja tu kwa mujibu wa Madaktari.

"Mbali na kuwa watanzania waliniombea sana lakini pia walinilea. Sijui kama kuna bei ambayo ninaweza kuwalipa wananchi wa Tanzania kwa upendo walionionyesha pamoja na kunitibu. nawashukuru kwa upendo wao. Nawaahidi kulipa hilo deni kwa kutoa uwakilishi unaostahili ukarimu wao," Lissu.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post