Friday, May 11, 2018

SUGU AJIFANANISHA NA MANDELA

  Malunde       Friday, May 11, 2018
Mbunge wa Mbeya Mjini (CHADEMA) Joseph Mbilinyi maarufu kama Sugu amesema anajiona shujaa baada ya kufanikiwa kutoka gerezani na kusema kuwa amepata hisia walizopitia viongozi waliofungwa kisiasa duniani.


Sugu amesema hayo jana Mei 10, 2018, wakati akiongea na vyombo vya habari nyumbani kwake Mjini Mbeya muda mfupi baada ya kuachiwa huru, na kusema kuwa yeye alifungwa kisiasa na ndiyo maana anajiona shujaa kwasabau ameingia katika kundi moja la vingozi wa zamani kama Hayati Nelson Mandela wa Afrika Kusini.


"Najisikia shujaa kuingia kundi la wafungwa wa kisiasa duniani, Mandela, Obasanjo, ingawa ni kwa muda mfupi lakini zile hisia alichokua anajisikia Mandela wakati yupo ndani, katikati ya usiku haupo na familia hizo hisia ninazo" amesema Sugu.


Sugu alitumia muda huo kuwapa pole wakazi wa jimbo la Mbeya mjini kwa sababu muda mrefu walimkosa Mbunge huyo na kudai kuwa yeye alifungwa kimwili ila wakazi wa jimbo hilo walifungwa mioyo.


Mbunge Sugu na Katibu wa Chadema kanda ya nyanda za juu kusini Emmanuel Masonga, waliachiwa huru jana Mei 10, 2018 baada ya kuhudumu katika Gereza la Ruanda mkoani mbeya kwa siku 73 ambapo taarifa ya Gereza hilo imedai wawili hao walitolewa kwa msamaha wa Rais John Magufuli alioutoa katika sherehe za siku ya muungano April 26, 2018.


February 26, 2018 Mahakama ya Hakimu mkazi Mbeya iliwatia hatiani Sugu na Masonga na kuhukumiwa kifungo cha miezi mitano jela kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli katika mkutano wa hadhara uliofanyika Disemba 30, 2017
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpyaHAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.bdkxfuvweev_drskoew
Previous
« Prev Post