Friday, May 18, 2018

SIMU YA NONDO ILIKUWA IKITUMIKA ALIPOTEKWA

  mtilah       Friday, May 18, 2018


 Shahidi katika kesi inayomkabili Mwenyekiti wa Mtandao wa Wanafunzi nchini, Abdul Nondo, amesema kuwa simu ya mtuhumiwa ilikuwa inatumika kipindi alichokuwa anadai kwamba ametekwa. 
Shahidi huyo ambaye amejulikana kwa jina la Abdul Kareem anayehusika katika kitengo cha makosa ya mtandao amesema kuwa simu ya Nondo ilikuwa ikitumika katika kipindi ambacho Mtuhumiwa alikuwa akidai ametekwa ingawa ameshindwa kuelezea ilikuwa ikitumika na nani kwa madai kuwa hana uwezo huo.
Akizungumza Wakili wa Abdul Nondo, B. Jebra Kambole amesema kwamba mbali na Shahidi Abdul Kareem, Koplo John ambaye ni mpelelezi katika kesi hiyo ametoa ushahidi wake ambao ni maelezo ya Nondo aliyoyatoa katika kituo cha polisi Iringa.
Wakili Kambole amesema kwamba licha ya serikali kuwa na mashahidi watano katika kesi hiyo, Juni 12-13 inategemea kuwepo na mashahidi wengine ambao bado hawajajulikana watakuwa wangapi.
Hakimu katika kesi hiyo John Mpitanjia ameahirisha kesi hiyo mpaka Juni 12 ambapo Mtuhumiwa Abdul Nondo ataendelea kuwa nje kwa dhamana.
Nondo anatuhumiwa kwa makosa mawili Kosa la kwanza ni kuchapisha taarifa za uongo mtandaoni Machi 7, 2018 akiwa Ubungo na kusambaza kwa kutumia mtandao wa WhatsApp kuwa yupo hatarini, kosa la pili ni kutoa taarifa za uongo akiwa mjini Mafinga kwa askari Polisi wa kituo cha Mafinga Wilayani Mufindi.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post