Saturday, May 12, 2018

MWIJAGE: NIKO TAYARI KUTOLEWA KAFARA AU KUPIGWA RISASI

  Malunde       Saturday, May 12, 2018
Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage amesema yuko tayari kutolewa kafara au kupigwa risasi kwa kuhubiri viwanda kwa kuwa tayari amefanikiwa kufufua viwanda 18 kati ya 56.


Pia amesema hana mamlaka ya kufuta baadhi ya viwanda vilivyobinafsishwa kwa wamiliki walioshindwa kuviendelea hadi hapo atakapopata baraka za Baraza la Mawaziri.


Mwijage ametoa kauli hiyo jana Mei 11 bungeni wakati akihitimisha bajeti ya wizara yake kwa kujibu hoja za baadhi ya wabunge.


Alisema kazi aliyopewa kuhusu viwanda vilivyobinafsishwa ni kuhakikisha viwanda vyote bila kujali mmiliki binafsi au serikali, vinafanya kazi vizuri ndiyo maana serikali inatambua mazingira wezeshi.


Amekiri kuwa ni kweli Tanzania katika takwimu za Benki ya Dunia haiko vizuri katika muktasari wa mazingira wezeshi ila ipo katika juu ya wastani wa asilimia 50.


“Sisi ni wa 137 kati ya nchi 190, lakini tupo juu ya asilimia 50. Sitaki kujivuna na hiyo nitafuata maelekezo yenu, ndio maana tunakuja bodi maalumu ambayo hizi taasisi mnazozilalamikia zitaanza kufanya kazi.


“Nimshukuru shangazi yangu Riziki Lulida (CUF), alisema nisiwe kondoo wa kafara, lakini hili la viwanda niko tayari kuwa kafara, nitahubiri viwanda anayetaka kunipiga risasi anipige risasi.


“Lulida unajua mtoto hakui kwa shangazi yake, nilipoelekezwa suala la viwanda, vilivyobinasishwa vilikuwa 156, nilifanya tathmini baada ya Rais kule Tanga aliponiambia namkwaza. Vilivyokuwa vinafanya kazi vizuri vilikuwa 62, vilivyokuwa havifanyi vizuri 56, vilivyokuwa vinasuasua 28, vilivyouzwa kwa vipuri mfano injini peke yake vilikuwa 10,” alisema.


Alisema baada ya kufanya kazi kwa muda wa mwaka mmoja kati ya viwanda 56, viwanda 18 vimekarabatiwa na vimeanza kazi.


“Na 35 vilivyobaki nitawasilisha kwa Spika haya ni mambo ya kitaalamu, vingine havina sifa ya kuitwa viwanda ila kwa mamlaka niliyonayo siwezi kuvifuta.


“Kwa mfano eneo la kiwanda cha kuunga trekta hapo Dar es Salaam nimeenda kufanya kukagua nikakuta wamejenga shopping mall nzuri kabisa inaajiri watu, inaitwa Quality Center, mimi mall naipenda kwa sababu inazalisha ajira, mnanishauri nikabomoe shopping mall?.


“Kulikuwa na viwanda vya kupasua mbao lakini sasa misitu imekwisha, sasa huyu mtu nimfanyeje nimuue huyo mtu? Vingine mali ya serikali mfano kiwanda cha maziwa mali ya NHIF (Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya), kiwanda cha serikali siwezi kukichukua.


“Nimemwambia ajenge kiwanda cha dawa. Yupo kwenye mchakato na suala dawa hivi namaliza kablda ya asubihi, wengine mnasema Mwijage you are not serious (hauko makini) siwezi kujiua,” alisema.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post