Wednesday, May 23, 2018

MUSUKUMA : NILIENDA KUVURUGA KWA LOWASSA

  Malunde       Wednesday, May 23, 2018
Mfanyabiashara na Mbunge wa Geita vijijini Joseph Musukuma amesema kuwa alienda kuvuruga harakati za kuwania Urais kwa aliyekuwa Mgombea wa Urais kupitia UKAWA Edward Lowassa ambaye alihama (CCM) baada ya kushindwa katika kura za maoni.

Musukuma ameyasema hayo kupitia kipindi cha Kikaangoni ya EATV inayorushwa kupitia ukurasa wake wa Facebook ambapo aliulizwa kuwa wakati wa kura ya maoni kumtafuta mgombea urais CCM alikuwa upande wa Lowassa na alivyohama aliendelea kuwa upande wake?.

Musukuma amejibu kuwa mgombea huyo hakuwa chaguo lake yeye alienda kwa ajili ya kazi maalum na alipokamilisha alipatikana Mgombea wa Urais kutoka Mkoani kwake.

“Unajua zingine ni mbinu tu za kibiashara hata wafanyabiashara wakubwa tunatumia mbinu hizo kwahiyo hata mimi nilienda tu kufanya kazi yangu nilipokamilisha akapatikana mgombea na ambaye ndiyo Rais wa sasa na anatoka kwetu Geita”, amesema Msukuma.

Mh. Musukuma ameongeza kuwa wabunge wengi wamekuwa hawana ujasiri wa kuzungumza ukweli kitu ambacho yeye anafanya kwa kujiamini.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post