KAULI YA STEVE NYERERE BAADA YA LULU KUTOLEWA GEREZANI

Taarifa za muigizaji maarufu nchini Elizabeth Michael”Lulu” kuachiwa huru siku ya leo Mei 14,2018 zimewafurahisha wengi baada ya kubadilishiwa adhabu na kumalizia adhabu yake nje ya gereza.

Mchekeshaji Steve Nyerere ambaye pia ni msemaji mkuu katika kitengo cha waigizaji (Bongo Movie) ni mmoja wa watu waliofurahishwa na taarifa hizo na kuonesha furaha yake kupitia ukurasa wake wa instagram.

“Lulu ni jambo la kushukuru sana kwani kila pito naamini Mungu supo pamoja nawe, nichukue nafasi hii kwa dhati kabisa kumshukuru Rais John Pombe Magufuli kwa msamaha huu naamini umefanya jambo jema sana Rais wangu. Nipongeze mahakama pia na wadau wote mliokuwa mnamuombea mwenzetu kutoka familia njoo Lulu tujenge tasnia yetu sasa”

Theme images by rion819. Powered by Blogger.