JINSI MBUNGE KISHOA ALIVYOPATA AJALI DODOMA


Mbunge wa viti maalumu (CHADEMA) wa Mkoa wa Singida Mheshimiwa Jesca Kishoa amepata ajali Jijini Dodoma leo Ijumaa Mei 11,2018 majira ya saa nne asubuhi. 

Akitoa taarifa za awali Afisa Habari wa CHADEMA Bw. Tumaini Makene amesema kwamba Mh. Kishoa amepata ajali asubuhi kwa kugongana na gari ndogo aina ya Pick Up alipokuwa njiani akielekekea kwenye majukumu yake ya kibunge.

Makene ameongeza kuwa ajali hiyo imetokea katika njia panda ya Area D mkoani huko.

Akizungumza akiwa amelazwa hospitali ya Bunge jijini Dodoma amesema:

“Hapa nimelazwa hospitali ya Bunge, nasikia maumivu katika mguu wa kulia lakini naendelea vizuri.

“Nimechomwa sindano ya kutuliza maumivu na ninaendelea vyema,” amesema Kishoa mke wa mbunge wa zamani wa Kigoma Kusini, David kafulila

Kuhusu mazingira ya ajali, Kishoa amesema; “katika mataa ya pale Area D, taa zilivyoruhusu, yule wa mbele yangu hakuwa ameonyesha kama atakata kona, sasa alivyokata kwa ghafla, mimi kufunga breki kwa nguvu ikafeli, nikaigonga kwa nyuma.


Theme images by rion819. Powered by Blogger.