Wimbo Mpya : PRINCE CHARLZ - NAKUTOGILWE... RNB KALI YA KISUKUMA


Charles Ndela 'Prince Charlz'

Msanii kutoka Kanda ya Ziwa, Charles Ndella 'Prince Charlz' ameachiwa wimbo mpya unaitwa Nakutogilwe (Nakupenda), alioimba kwa mahadhi ya taratibu RnB.

Wimbo huu ameufanyia Black Lebo Studio kupitia mikono ya Producer 9Hourz.

Prince Charlz amewashangaza wapenzi wengi wa Muziki wa RnB kwa kuimba kwa kutumia Lugha ya Kisukuma lakini kwa ufundi wa hali ya juu.

 Akizungumza na Malunde1 Blog, Mratibu wa kazi za Charles Ndela, Gabriel Ng'osha amesema wamejipanga kufanya tour maalumu kwa mikoa ya Kanda ya Ziwa kwa ajili ya kusambaza muziki wake.

Amesema hadi sasa Ndela ameshafanya kazi kadhaa ikiwemo Sensemamalunde, Kisura wa Nzega, Napendaga na zinginezo ambazo ameimba kwa lugha ya Kisukuma na Kiswahili 

"Prince Charlz ni msanii ambaye anaweza kuimba mitindo mbalimbali ya muziki, hivyo wadau wa muziki wa Kanda ya Ziwa na kwingineo ninaomba wampokee msanii mzalendo. Ndela anatamani kufanya kolabo na wasanii mbalimbali akiwemo Saida Karoli, Mrisho Mpoto, Wanne Star, Diamond, Alikiba, Joh Makini, Vanessa na wengineo," alisema Ng'osha.

SIKILIZA NGOMA HII HAPA CHINI

Theme images by rion819. Powered by Blogger.