SERIKALI YAWASIMAMISHA KAZI MAWAKILI SITA MAKOSA YA NIDHAMU

Waziri wa Katiba na Sheria, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema mawakili sita wamesimamishwa kufanya kazi ya uwakili kwa miezi sita hadi miaka mitano kwa makosa ya nidhamu.


Kabudi ameyasema hayo leo bungeni wakati akiwasilisha mipango wa makadirio ya bajeti ya wizara ya Katiba na Sheria.


Amesema uamuzi huo umetolewa na kamati ya nidhamu ya mawakili baada ya kupokea malalamiko hayo


Profesa Kabudi, amesema kamati hiyo ilipokea malalamiko 18 ya mawakili kwa mwaka wa fedha 2017/2018 na hivyo kufanya jumla ya malalamiko yaliyokuwa mbele ya kamati kufikia 48.


“Katika kipindi hicho, malalamiko 22 yalisikilizwa na kutolewa uamuzi ambako mawakili sita wamesimamishwa kazi ya kufanya uwakili kwa muda wa miezi sita hadi miaka mitano,” amesema.


Ametoa wito kwa mawakili wote nchini kutekeleza majukumu yao kwa uadilifu wakitambua kuwa wao ni maofisa wenye dhamana kubwa ya kufanikisha utoaji wa haki kwa wakati.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553
Previous Post Next Post