Wednesday, April 25, 2018

BINTI WA MIAKA 20 AMUUA NDUGU YAKE WA MIAKA MIWILI KISHA KUMFICHA UVUNGUNI

  Malunde       Wednesday, April 25, 2018
Mtoto wa miaka miwili amefariki dunia baada ya kuchomwa na kitu chenye ncha kali kitovuni na kuwekwa uvunguni mwa kitanda nyumbani kwao Kigamboni.


Kamanda wa Polisi Mkoa wa Temeke, Emmanuel Lukula amesema  tukio hilo limetokea juzi Jumatatu ambapo inadaiwa kuwa binti wa miaka (20) alimchoma mtoto huyo kwenye kitovu kwa kutumia kitu chenye ncha kali na kumficha uvunguni.

“Ni kweli tukio hilo limetokea juzi, aliyefanya hilo tukio ni binti wa miaka 20 ambaye ni ndugu wa mama wa marehemu. Si mfanyakazi wa ndani kama wengine wanavyodai, alimchoma huyo mtoto na kumlaza kifudifudi uvunguni kisha akaondoka,’’ ameeleza Kamanda Lukula na kuongeza:

“Sijapata majina sahihi maana nilielekeza niletewe na bado sijaletewa lakini tukio hilo ni la kweli.’’

Kamanda Lukula amesema baada ya huyo binti kufanya tukio hilo aliondoka nyumbani hapo.

“Huyo binti baada ya kufanya hilo tukio alikwenda kwa mwanaume anayedaiwa kuwa na uhusiano wa kimapenzi na baada ya mama wa mtoto kurudi kazini hakumkuta nyumbani,’’amesema

Baada ya uchunguzi wa polisi, binti huyo alikamatwa na alikwenda kuwaonyesha alipomuweka mtoto uvunguni mwa kitanda.

Kamanda Lukula amesema kwa sasa taratibu nyingine za kisheria zinaendelea baada ya mtuhumiwa kukamatwa.

Na Emmanuel Mtengwa, Mwananchi
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post