BILIONEA ATANGAZA KUNUNUA UWANJA WA TAIFA

Mmiliki wa klabu ya Fulham, Shahid Khan, amesema ana tumaini mpango wa kununua Uwanja wa Wembley unaotumika kama uwanja wa taifa wa England, kutoka kwa Chama cha Soka cha England FA utakamilika ndani ya wiki nane hadi 12 zijazo.
Bilionea huyo mzaliwa wa Pakistani ambaye ni raia wa Marekani, amesema atalipa kiasi cha £ 900m zaidi ya Shilingi Trioni mbili kwaajili ya kukamilisha mpango huo. Hata hivyo hajaweka wazi kama uwanja huo utakuwa ndio uwanja wa Fulham.

''Ninaamini tutakubaliana na FA ndani ya wiki 8 hadi 12 na biashara itakwenda vizuri kwasababu uwanja utaendelea kuitwa jina hilo (Wembley), kwa kuheshimu utamaduni wa England lakini pia timu ya taifa ya England itaendelea kuutumia'', amesema.

Khan mwenye umri wa miaka 67 pia anamiliki klabu ya Jacksonville Jaguars inayoshiriki katika ligi ya soka la Marekani (American Football). Ameahidi kama atamiliki uwanja huo timu hiyo itakuwa na mechi za kirafiki zaidi ya 10 na timu za EPL kila msimu.

Kwasasa Wembley unatumika kama uwanja wa nyumbani wa Tottenhma Hotspur ambayo ipo kwenye matengenezo ya uwanja wake mpya unaotarajiwa kukamilika mwaka huu na kuanza kutumika msimu wa 2018/19.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527