Monday, March 19, 2018

UJERUMANI NA DENMARK KUWEKEZA TANZANIA

  Malunde       Monday, March 19, 2018
Rais John Magufuli ameeleza kuwa siku za hivi karibuni atakutana na Wakurugenzi Watendaji wawili kutoka nchi za Ujerumani na Demark ambao watakuja kufanya uwekezaji nchini.


Kauli hiyo ameitoa leo Machi 19, 2018 wakati wa mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara, uliobeba maudhui ya ‘Tanzania ya Viwanda na Ushiriki wa sekta binafsi nchini.’


Rais Magufuli ameeleza kuwa watakuja kufanya uwekezaji wa kiwanda kipya cha Petroli Kemikali (Petrol Chemical Plant) ambacho kitakuwa na thamani ya Dola za Marekani Bilioni 1.92 ambayo ni sawa na takriban Shilingi za Kitanzania Trilioni 4.56.


Ameeleza kuwa kiwanda hicho kinatarajiwa kutoa ajira kwa Watanzania zaidi ya 4000 katika eneo la Kilwa kwaajili ya kutengeneza mbolea ambayo itauzwa ndani pamoja na nje ya nchi kwa kutumia gesi iliyopo nchini.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post