TIGO TANZANIA NA UBER WAUNGANA KULETA OFA MPYA, MURUA KWA WATEJA WA DAR ES SALAAM


Mkurugenzi Mkuu wa Tigo Tanzania, Simon Karikari akipeana mikono na Meneja Mkuu wa Uber Afrika Mashariki, Loic Amado mara baada ya kuingia makubaliano ya kipekee yatayowafaidisha watumiaji wa Tigo wakaotumia huduma za usafiri za Uber kwa kutumia Uber App bure. Kulia ni Mkurugenzi Mkaazi wa Uber Tanzania, Alfred Msemo na kushoto ni Afisa Mkuu wa Kitengo cha Huduma za Fedha wa Tigo, Hussein Sayed kwenye hafla iliyofanyika jijini Dar Es Salaam jana. 
***

Dar es Salaam, 19 Machi, 2018. Kampuni inayoongoza kwa mageuzi ya kidigitali nchini, Tigo Tanzania imeingia katika makubaliano ya kipekee na kampuni ya kiteknologia ya Uber. Kuanzia leo, wateja wote wa Tigo watatumia huduma za Uber App bure! Makubaliano haya ya aina yake yatawafaidi watumiaji wa huduma za usafiri za Uber pamoja na madereva waliojiunga na mfumo huo. 


“Tigo ni nembo pana ya biashara katika soko la Tanzania na tuna wajibu wa kuzindua njia bora zaidi kwa wateja kujumuika katika maisha yanayowazingira. Makubaliano haya na Uber yanaboresha bidhaa na huduma ambazo wateja wetu wanafurahia katika maisha yao ya kila siku,” Mkurugenzi Mtendaji wa Tigo, Simon Karikari alisema. 

Naye Alfred Msemo, Mkurugenzi wa Uber alisema, “Tunafurahia makubaliano haya na Tigo yatakayowawezesha watumiaji na madereva wa huduma za Uber waliojisajili na mtandao wa Tigo kutumia huduma ya Uber App bure kwenye simu zao za mkononi bila tozo lolote la gharama za data. Uber ni mfumo wa simu za kisasa unaowezesha watu kusafiri kutoka sehemu moja hadi nyingine kwa kubonyeza kitufe tu! Lengo kuu la Uber ni kuwezesha usafiri salama, wa uhakika na kwa gharama nafuu kwa kila mtu, kila sehemu. Makubaliano haya yatawahamasisha maelfu ya wakaazi wa Dar es Salaam ambao wamejisajili na mtandao wa Tigo kutumia Uber App kwa ajili ya huduma za usafiri jijini Dar es Salaam,’ Msemo alibainisha. 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527