Thursday, March 1, 2018

RUFAA YA SUGU IMETUA MAHAKAM TUU

  mtilah       Thursday, March 1, 2018


 Rufaa ya kupinga hukumu ya kifungo cha miezi mitano jela iliyotolewa kwa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga imewasilishwa Mahakama Kuu Kanda ya Mbeya.

Akizungumza leo Machi 1, 2018 mmoja wa mawakili wa Sugu, Faraji Mangula amesema  tayari maombi ya rufaa yao yamepokewa leo  mchana na kupewa kumbukumbu namba 29/2018.

“Tayari rufaa yetu imeshapokewa Mahakama Kuu (Mbeya) na tunachosubiri  ni kupangiwa tarehe ya kuanza kusikiliza tu, ila tunachoshukuru watu wa Mahakama hii wapo vizuri kushughulikia suala hili,” amesema Mangula.

Mbali na kukata rufaa hiyo, lakini pia mawakili hao wanakusudia kuomba dhamana kwa wateja wao  ili waweze kuwa nje katika kipindi ambacho wanakuwa wanasikiliza rufaa yao.

Sugu na Masonga walihukumiwa baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutumia lugha ya fedheha dhidi ya Rais John Magufuli.

Wawili hao walitoa kauli hiyo Desemba 30 mwaka jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika kwenye viwanja vya Shule ya Msingi Mwenge jijini Mbeya.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post