POLISI WATUHUMIWA KUUA KIJANA MUUZA MACHUNGWA

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya, linatuhumiwa kuhusika na mauaji ya kijana muuza machungwa katika soko la Sido ambaye ni mkazi wa Mtaa wa Iyela II, jijini Mbeya, anayesadikiwa kufariki katika mazingira ya kutatanisha.

Kifo cha kijana huyo aliyefahamika kwa jina la Allen Mapunda (20), kimetokea wakati ndugu wa marehemu wakiwa katika Hospitali ya Rufaa ya Kanda ya Mbeya ambapo imeelezwa kuwa kabla ya umauti marehemu alikamatwa Machi 24, 2018 majira ya saa 4 usiku katika eneo la kucheza 'pull table' lililopo Mtaa wa Maendeleo, na kumpeleka hadi kituo kikuu cha Polisi ambapo alikaa kwa siku moja na kesho yake alidhaminiwa na ndugu ambao waliamua kumpeleka hospitali kwa ajili ya matibabu kutokana na majeraha aliyopata.

Kwa mujibu wa mama mlezi, Alice Mapunda amesema marehemu alionekana na majereha mkononi na kichwani ambako alikuwa akivuja damu huku akilalamikia kupata maumivu.

Akizungumzia tukio hilo Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, Mohammed Mpinga amesema uchunguzi juu ya kifo wa kijana huyo unaendelea na kwamba taarifa rasmi ataitoa mara baada ya uchunguzi kukamilika kwa vyombo vya habari ili waweze kufahamu ukweli wa tukio hilo ulivyo.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527