NEY WA MITEGO : MIMI NDIYO CHANZO CHA NYIMBO KUFUNGIWA TANZANIA

Emmanuel Elibariki mwanamuziki wa Tanzania


Mwanamuziki wa kizazi kipya Emmanuel Elibariki, alimaarufu kama Ney wa Mitego amesema yeye ndio chanzo cha maamuzi ya nyimbo kufungiwa Tanzania.

Nyimbo zaidi ya kumi zilitangazwa na Mamlaka ya Mawasiliano kupigwa marufuku kuchezwa katika radio nchini Tanzania.

Ney wa mitego akiongea na BBC,amesema

'Wakati mwingine naona kuwa sababu ya kufungiwa kwa miziki hii ni mimi na wengine wanawekwa kama chambo kwa kuwa kati ya nyimbo zote hizo,nyimbo mpya peke yake ni yangu tu ambayo imetoka wiki mbili zilizopita na video ina wiki moja tu" Ney wa Mitego.

Hata hivyo hii sio mara ya kwanza kwa mwanamuziki huyo kupata misukosuko katika muziki wake.

Mnamo mwezi machi mwaka jana Ney wa Mitego aliwahi kukamatwa na jeshi la polisi la Tanzania kwa kosa la kuimba wimbo unaokashifu serikali lakini inakumbukwa kuwa mwanamuziki huyo aliwahi kupewa onyo kuhusiana na mavazi yake.

Huku wanamuziki wengine bado hawakuwa tayari kutoa maoni yao.

Wakati huo huo , hii leo, msanii wa bongo fleva, Roma Mkatoliki aliyefungiwa wimbo wake mpya wa 'kibamia' kwa sasa amefungiwa na Naibu Waziri wa habari,sanaa,utamaduni na michezo Juliana Shonza kutojihusisha na tasnia ya muziki kwa takribani miezi sita mara baada ya kukiuka kurekebisha wimbo huo .

Baadhi ya wananchi walioongea na BBC,walikuwa na maoni tofauti.Maoni ya watanzania
Meneja wa mawasiliano wa TCRA,Semu Mwakyanjala amelizungumzia suala la muda na kusema kuwa 'wakati wa kufungia haujalishi kikubwa ni nyimbo hizo zilizofungiwa ni hazina maadili.'

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527