Wednesday, March 14, 2018

MWANAFIZIKIA STEPHEN HAWKING AFARIKI DUNIA

  Malunde       Wednesday, March 14, 2018

Prof Stephen Hawking, mwanafizikia maarufu duniani, amefariki dunia akiwa na miaka 76, familia yake imetangaza.

Mwingereza huyo alifahamika sana kwa kazi yake ya kisayansi kuhusu uwepo wa eneo katika anga za juu ambapo nguvu za mvutano huwa za juu sana kiasi kwamba miali nururishi au hata mwanga hauwezi kuponyoka.

Kwa Kiingereza, eneo hilo hufahamika kama 'Black Hole'.

Alitumia hilo katika kujaribu kufafanua kuhusu asili ya vitu vyote duniani na angani.

Alikuwa mwandishi wa vitabu kadha maarufu vya sayansi kikiwemo A Brief History of Time (Historia Fupi kuhusu Wakati).

Watoto wake, Lucy, Robert na Tim, wamesema: "Tumehuzunishwa sana kwamba baba yetu mpendwa ametuacha."

"Alikuwa mwanasayansi muhimu na mtu wa kipekee ambaye kazi zake na mchango wake vitaendelea kukumbukwa kwa miaka mingi."

Mambo muhimu kuhusu maisha ya Stephen Hawking

Alizaliwa 8 Januari 1942 Oxford, England

Alipata nafasi chuo kikuu cha Oxford kusomea sayansi ya mambo
 asilinia mwaka 1959, kabla ya kwenda kusomea shahada ya uzamifu chuo kikuu cha Cambridge

Kufikia 1963, alipatikana na ugonjwa ulioathiri mfumo wake wa neva na mawasiliano mwilini. Madaktari walimwambia hangeishi zaidi ya miaka miwili.

Alieleza nadharia yake kwamba 'black hole' kutoa "Miali ya Hawking" mwaka 1974

Alichapisha kitabu chake A Brief History of Time mwaka 1988. Nakala zaidi ya 10 milioni za kitabu hicho ziliuzwa.

Maisha yake yaliangaziwa kwenye filamu ya The Theory of Everything ya mwaka 2014 ambapo Eddie Redmayne aliigiza nafasi ya mwanasayansi huyo

Stephen Hawking alipokuwa na miaka 22 pekee aliambiwa na madaktari angeishi miaka mingine miwili pekee baada yake kupatikana na ugonjwa nadra sana wa mfumo wa neva.

Ugonjwa huo ulimfanya kulemaa na kulazimika kutumia kiti cha magurudumu.

Nyakati za mwisho za maisha yake, alikuwa hawezi kuzungumza ila kwa kutumia kifaa cha kufasiri mawazo yake na kuyageuza kuwa sauti.
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post