MAALIM SEIF ASEMA WARAKA MZITO KKKT UMEMFARIJI


Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amelipongeza Baraza la Maaskofu la Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT) kwa kutoa waraka mzito wa ujumbe wa Sikukuu ya Pasaka.


Waraka huo ulitolewa mwishoni wa wiki iliyopita ambao mbali na kuzungumzia masuala ya kiroho, umetaja changamoto tatu na kuzifikisha kwa waumini wake “ili ziongeze mzigo wa kuliombea taifa letu na viongozi wake.”


Changamoto zilizotajwa katika waraka huo uliopewa jina la “Taifa Letu Amani Yetu” na kusainiwa na maaskofu 27 wa kanisa hilo nchini ni hali ya kijamii na kiuchumi, maisha ya siasa na masuala mtambuka likiwamo suala la Katiba Mpya.


Akizungumza leo Machi 26, 2018 jijini Dar es salaam wakati akisoma maazimio manne ya Kamati ya Utendaji ya Taifa ya chama hicho iliyokutana leo, Maalim Seif amesema anafarijika kuona viongozi wa dini wanakemea mambo ambayo hayaendi sawa nchini.


"Nimefarijika kuona viongozi wa taasisi za dini wakizungumza pale ambao wanaona mambo hayaendi sawa. Tusitafsiri kwamba wanafanya siasa, hapana ni haki yao kukemea, "amesema Maalim Seif.


Amesema angetamani kuona viongozi wengine wa dini wakionyesha misimamo kama maaskofu hao.

Na Kelvin Matandiko Mwananchi

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527