Wednesday, March 28, 2018

MAADHIMISHO YA UPANDAJI MITI KITAIFA KUFANYIKA KISHAPU MKOANI SHINYANGA

  Malunde       Wednesday, March 28, 2018

Maadhimisho ya upandaji miti kitaifa yanatarajia kufanyika wilayani Kishapu mkoani Shinyanga kuanzia Aprili 3,2018 hadi Aprili 5,2018.

Akitoa taarifa ya maadhimisho hayo ya upandaji miti kwa vyombo vya habari ,leo Machi 28,2018   Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Zainabu Telack,alisema miongoni mwa shughuli zitakazofanyika wakati wa maadhimisho hayo ni kutoa elimu ya utunzaji wa mazingira kwa wananchi na  upandaji miti ambapo jumla ya miti 232,000 itapandwa wilayani humo. 

Telack amesema shughuli kubwa itakuwa ni upandaji miti ambapo kila familia itakabidhiwa miti kwa ajili ya kupanda kwenye kaya zao pamoja na kuitunza lengo likiwa ni kuondoa hali ya jangwa wilayani Kishapu na kuifanya kuwa ya kijani. 

“Katika maadhimisho hayo siku ya kilele chake April hiyo 5,2018 mgeni rasmi anatarajiwa kuwa
Waziri wa Maliasili na Utalii Dr. Hamisi Kigwangalla, naomba wananchi wajitokeze kwa wingi ili tushiriki kwa pamoja kupanda miti na kupewa elimu ya utunzaji mazingira na faida zake,” amesema Telack. 

Na Marco Maduhu - Malunde1 blog & Shinyanga News blog
Usikubali kupitwa na habari..Pakua App ya Malunde1 blog HAPA Ili tuwe tunakutumia habari moja kwa moja Kwenye Simu yako
Loading...
logoblog

Kama Una Habari,Picha,Video,Tangazo n.k Wasiliana Nasi Simu/WhatsApp +255 757 478 553 ,0625 918 527

Malunde 1 blog Ipo PlayStore....Pakua App yetu mpya HAPA Upate Habari Mpya Moja Kwa Moja Kwenye Simu yako..Utasoma habari hata kama hauna MB..Bofya Hapa
https://play.google.com/store/apps/details?id=com.malunde.blog
Previous
« Prev Post