KIJANA AMUUA MAMA MKWE,AMKATA PANGA MKEWE KISHA KUJILIPUA KWA PETROLI

Kijana aliyefahamika kwa majina ya Joseph Medardi (32) mkazi wa Nyakahanga Wilaya ya Ngara mkoani Kagera amemuua mama mkwe wake Elizabeth Simon (70) kwa kumkata kata mapanga na kumjeruhi mkewe Elice Joseph (28) kisha na yeye kujimwagia petroleum.


Kijana huyo amefanya tukio hilo kwa kile kilichoelezwa kuwa alikuwa na matatizo na mkewe kuhusu suala la unyumba jambo ambalo lilimpelekea kumrudisha mkewe huyo nyumbani kwa mama yake, ambapo amekaa huko takribani wiki tatu, siku moja kabla ya kikao cha kuwasuluhisha wanandoa hao ndipo kijana huyo ametekeleza mauaji hayo.


Mtoto wa marehemu Elizabeth Simon (70) ambaye ni Mchungaji Ezekia Simon amesimulia jambo hilo kwa undani zaidi na kusema kuwa chanzo cha yote hayo kuwa ni matatizo ya unyumba na kudai kuwa kijana huyo ambaye yeye ni shemeji yake alionekana amekuja na kusudio la kuwaua wote yaani mama yake pamoja na mdogo wake huyo ambaye amejeruhiwa tu.


"Kisa cha kifo cha mama kimetokana na Mume wa dada kutoelewana katika habari za unyumba. Walikuwa na mgogoro kwa maana hiyo ikapelekea kumfukuza mkewe hivyo alikuja hapa yapata kama takribani wiki tatu yuko hapa nyumbani na baada ya hapo mimi kama Mkuu wa familia nilijaribu kutafuta njia ya kuwasuluhisha hivyo tarehe ambayo tulipanga kukutana ilikuwa jana ingawa hatukufanikiwa kukutana baada ya mzazi wa kijana kusema hakupata taarifa, matokeo yake yule kijana ndiyo amekuja akawashambulia mama pamoja na dada na kusababisha mauti ya mama" Alisema Mchungaji Simon na kuendelea;


"Yule kijana alikuja kwa lengo la kuua wale na yeye kujiua kwa sababu alipowashambulia na kuwajeruhi yeye alijimwagia Petroleum na kujichoma moto ndani ya nyumba hii hii"

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527