ASKARI POLISI AFARIKI BAADA YA KUMGONGA KWA BAISKELI MTEMBEA KWA MIGUU

Askari polisi wa Kituo cha Babati mkoani Manyara, Boniface Masunga (32) amefariki dunia baada ya baiskeli aliyokuwa akiendesha wakati akielekea kazini kumgonga mtembea kwa miguu.


Baada ya kumgonga mtu huyo, askari huo aliangukia kichwa na kufariki dunia papo hapo.


Akizungumza jana Jumamosi Machi 24, 2018, Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Manyara, Agostino Senga alisema tukio hilo limetokea Ijumaa katika barabara kuu ya Babati-Singida.


Alimtaja aliyegongwa kuwa ni Awadhi Ashraf (20) mkazi wa mjini Babati na kwamba, chanzo cha ajali hiyo ni Ashraf ambaye ni fundi ujenzi kuingia barabarani bila kuchukua tahadhari.


"Huyo fundi alikuwa anaingia kwenye barabara kuu ya lami bila kuchukua tahadhari, hivyo akagongwa na baiskeli aliyokuwa anaendesha polisi huyo," alisema Kamanda Senga.


"Tukio hilo lililotokea ghafla sana kwani alivyomgonga aliangukia kichwa na kuanza kutokwa damu masikioni.”


Hata hivyo, baadhi ya mashuhuda wa ajali hiyo walishangazwa na ajali hiyo kwani hawajawahi kuona mtu akagongwa na baiskeli na mwendeshaji kufa.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com au WhatsaApp: + 255 757 478 553 au 0625 918 527